IQNA

Waislamu China

Msomi  wa Qurani wa China atembelea maonyesho ya Tehran

18:11 - March 25, 2024
Habari ID: 3478572
IQNA - Sheikh Yaqub Mashidu ni msanii wa Kichina na mfasiri wa Qur'ani ambaye amehudhuria Awamu ya 31 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran.

Alishiriki katika kongamano la wataalamu wa Hauza (seminari za Kiislamu)  katika maonyesho hayo Jumamosi jioni.

Mashidu alibainisha katika kongamano hilo kuwa hivi sasa anaandika tafsiri ya Qur'ani kwa kuzingatia utamaduni wa Wachina.

Uandishi wa tafsiri hiyo ya Qur'ani iliyopewa anuani ya Al-Wa’z al-Hakim Lil-Quran al-Karim, unaendelea na nusu yake imakamilika, alisema.

Ameongeza kuwa kwa sababu ya kutopata tafsiri za Qur'ani za madhehebu ya Shia ametegemea zaidi Tafsirs za Kisunni katika tafsiri yake.

Mwanazuoni huyo wa China amesema anayaona maonyesho hayo ya Qur'ani ya Tehran kuwa ni fursa nzuri ya kujenga mafungamano na kuendeleza uhusiano wa kielimu katika nyanja za Qur'ani.

Kwingineko katika maelezo yake, Sheikh Mashidu aligusia mbinu za kujifunza Qur'ani miongoni mwa Waislamu nchini China, akisema pamoja na kujifunza Quran kupitia Kiarabu, watoto Waislamu pia wanajifunza lugha ya Kifarsi.

Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa Jumatano Machi 20 katika ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA).

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Huonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

3487707

 

captcha